Thursday, September 3, 2015

KWA HAPA, SIMBA HAWAKO VIBAYA...




SIMBA imeonekana kuwa na viungo wengi wenye ubora, lakini pia Yanga na Azam nazo zikiwa si haba katika safu hiyo ikiwa ni baada ya usajili uliofanywa kuanzia wachezaji wa kigeni hadi wazawa tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 12, mwaka huu.

Katika usajili wao wa msimu ujao, Simba iliwanasa viungo, Justuce Majabvi kutoka Zimbabwe, Peter Mwalyanzi (Mbeya City), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla, Awadh Juma na Issa Abdallah aliyepandishwa kutoka timu B.

Hao wameungana na wa msimu uliopita kama Jonas Mkude, Said Ndemla, Awadh Juma na wengineo kuifanya safu ya kiungo ya Wekundu wa Msimbazi hao kuimarika.

Kwa upande wao, Yanga nao walifanikiwa kusajili viungo wapya wakiwanasa Thaban Kamusoko, Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya walioungana na Salum Telela, Haruna Niyonzima, Said Juma, Andrey Coutinho na Simon Msuva waliokuwapo kundini msimu uliopita.

Azam, wao walisajili viungo watatu tu ambao ni Jean Mugiraneza kutoka Rwanda, Ame Ali (Mtibwa Sugar) na Ramadhan Singano ‘Messi’ (Simba), huku ikimpandisha kinda wao, Sarid Mussa.
Chanzo:Bingwa.

0 Responses to “KWA HAPA, SIMBA HAWAKO VIBAYA...”

Post a Comment

More to Read