Thursday, September 3, 2015

MAN UNITED WAANIKA KIKOSI CHA UEFA CHAMPIONS LEAGUE, HATIMA YA DE GEA HII HAPA...






Manchester United wametaja kikosi kitakachocheza hatua ya makundi ya Champions League, huku wakijumuisha jina la golikipa David De Gea ambaye uhamisho wake kwenda Real Madrid ulikwama dakika za mwisho za dirisha la majira ya kiangazi huko Hispania. 

Kwasasa De Gea yuko na kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania inayojiandaa na mchezo wa mwisho mwa Juma hili wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016 nchini Ufaransa.

Hata hivyo, Mhispania mwenzake, Victor Valdes hajaingizwa kwenye kikosi hicho chenye wachezaji 26.


0 Responses to “MAN UNITED WAANIKA KIKOSI CHA UEFA CHAMPIONS LEAGUE, HATIMA YA DE GEA HII HAPA...”

Post a Comment

More to Read