Thursday, September 10, 2015
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KINYAMA MKOANI ARUSHA AFIKISHWA MAHAKAMANI.
Do you like this story?
Mtuhumiwa wa mauaji katika Hoteli
ya A Square Belmont jijini Arusha, Elijus
Lyatuu ,
ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano wa masomo ya falsafa katika Chuo cha
Kanisa la Katoliki Segerea jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani na
kusomewa shtaka la mauaji.
Mtuhumiwa huyo, alifikishwa mahakamani
jana saa 4:30 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ndani ya gari aina
ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1434.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Lilian
Mmasi, alidai mbele ya Hakimu Nestory Barowa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Arusha, kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa la kumuua Alfred Kimbaa
maarufu kwa jina la Mandela (18), Agosti 30, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Belmont
jijini hapa.
Alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo
kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo, aliomba mahakama hiyo
kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja kesi hiyo kutokana na madai kuwa
upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Kwa upande wake, hakimu Baro alimweleza
mtuhumiwa huyo kuwa kesi inayomkabili haina dhamana, hivyo atalazimika
kuendelea kukaa mahabusu hadi shauri hilo litakapoanza kusikilizwa.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba
23, mwaka huu itakapokwenda kwa ajili ya kutajwa tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KINYAMA MKOANI ARUSHA AFIKISHWA MAHAKAMANI.”
Post a Comment