Tuesday, June 21, 2016
GEPF YAZINDUA MPANGO WA BODA BODA KUINGIA MFUKO WA MAFAO YA UZEENI JIJINI MBEYA
Do you like this story?
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano,Aloyce Mtukamazina Akizungumza na Waandishi wa Habari lengo la kuja Mbeya. |
KATIKA
mkakati wa kuboresha maisha kwa madereva wa bodaboda nchini
Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF) imeanzisha na mpango mpya wa kuinua
ukia na lengo la kuiwezesha jamii hiyo kuishi maisha bora na yenye
malengo ya endelevu.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi za Mfuko huo
Mkoa wa mbeya Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano,Aloyce
Mtukamazina amesema kuwa mpango wa kuwawezesha madereva wa bodaboda
uliopewa jina la Bodaboda Scheme unatarajiwa kuzinduliwa Juni 23 mwaka
huu katika mkutano wa wadau wa Mfuko huo utakaofanyika kila mwaka na
mwaka huu unafanyika jijini Mbeya.
Mtukamazina amesema Mfuko umekuja na mpango huo mpya baada ya Mafao
mapya manee yaliyozinduliwa mwaka jana ya Fao la Uzazi,Mkopo wa
Elimu,Mkopo wa kuanza Maisha na Mkopo wa kujikimu iliyowalenga zaidi
vijana wanaoanza kazi kuonesha mafanikio makubwa.
Alisema ili kuendelea kuwezesha jamii ya vijana ambayo kimsingi ndiyo
nguvu kazi ya Taifa,mfuko umeona haja ya kutanua wigo wa fursa kwa
kada hiyo ambapo sasa kupitia Juma la GEPF wameamua kuutambulisha
rasmi mfuko wa mafao wa Bodaboda Sceme.
Alisema kupitia mafao hayo,madereva wa bodaboda wataweza kunufaika
kupitia kujiwekea akiba na pia fursa ya kupata mkopo muda mfupi tu
baada ya kuwa mwanachama wa GEPF.
"Baada ya kuanizisha mifuko kadhaa hUko nyuma sasa tumekuja kivingine
kabisa,tumewalenga wajasiriamali ambao hawapo katika mfumo rasmi ajira
ambao takwimu zinaonesha ndiyo nguvu kazi kubwa ya taifa,kwanza
tumeangalia kundi la sekta ya usafirishaji na hapa tunawalenga zaidi
madereva wa Bodaboda,Bajaji na madereva wa daladala"alisema
Ntukamazina.
Alisema kupitia Bodaboda Scheme pia madereva wa bodaboda wataweza
kujiwekea akiba itakayowapa fursa ya kupata mafao yao kama ilivyo kwa
wastaafu wa ajira zilizo rasmi hatua itakayowapa wakati mzuri baada ya
kustaafu kazi yao.
Aidha,Ntukamazina alisema pia Alisema GEPF ina mkakati wa kuwawezesha
madeereva hao kujiunga katika fao la Afya ili kuwawezesha kupata
matibabu pale wanapopatwa na matatizo ya kiafya ikiwemo majeraha ya
ajali sambamba na familia zao.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ GEPF YAZINDUA MPANGO WA BODA BODA KUINGIA MFUKO WA MAFAO YA UZEENI JIJINI MBEYA”
Post a Comment