Tuesday, June 21, 2016

Usajili wa Victor Wanyama wakamilika kwa £13.5 kujiunga na Tottenham



Kiungo mkabaji kutoka nchini Kenya Victor Wanyama amesafiri kutoka Nairobi mpaka London siku ya Jumapili kwa ajili ya ya kumalizia vipimo ya afya ili kukamirisha taratibu za usajili na hivyo kuwa tena chini ya kocha wake wa zamani Mauricio Pochettino.
 


Wanyama atajiunga katika safu ya kiungo wa kati ambapo atakuwa akishirikiana na Eric Dier pamoja na Mousa Dembele ambao wote kwa sasa wapo katika timu zao za Taifa katika mashindano ya Euro 2016.

“Ni ngumu sana kuachana na klabu ambayo umezoea tamaduni pamoja na wapenzi na mashabiki wake, lakini ni ndoto ya kila mcheza mpira wa miguu kucheza katika kiwanga cha juu na katika moja ya ligi bora zaidi kama ligi ya mabingwa Ulaya (Champions league), nitawamiss mashabiki zangu pamoja na wapenzi wote wa Southampton ingawa najua kuwa watakuwa waelewa katika uamuzi wangu huu” - Wanyama
 


0 Responses to “Usajili wa Victor Wanyama wakamilika kwa £13.5 kujiunga na Tottenham”

Post a Comment

More to Read