Tuesday, June 21, 2016

Jamaa ashitakiwa kujaribu kumwuua Donald Trump



Kijana wa miaka 20, Steven SandFord amewekwa chini ya ulizi mkali baada ya kufanya jaribio la kumuua Donald Trump katika moja ya mkutano wake wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Mystere jijini Las Vegas.

Kitengo cha waangalizi wa hali ya Usalama wanchini Marekani wanaelezea jinsi SandFord alivyojaribu kutimiza azama yake ya kwa kuwaambia walinzi wa Trump kuwa alitaka kupiga picha pamoja na kiongozi huyo.

Kijana huyo alikamatwa baada ya kujaribu kuchukua silaha aliyokuwa nayo askari polisi aliekuwepo katika mkutano huo.

Kwa maelezo ya mwanzo kutoka kwa SandFord anasema kwa amekuwa akipanga kufanya tukio hilo kwa muda wa mwaka mmoja kwa sasa na alikuwa tayari ameshakata tiketi kwenye mkutano wa Trump Phoniex ambao umesogezwa mbele zaidi kwa siku moja.

Zaidi ya watu 1500 walihudhuria mkutano huo wa hadhara ambao ulifanyika katika kumbi za Mystere.


0 Responses to “Jamaa ashitakiwa kujaribu kumwuua Donald Trump ”

Post a Comment

More to Read