Friday, June 17, 2016
SERIKALI YATENGA TSH. BILIONI 5 KUJENGA JENGO LA MIONZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
Do you like this story?
SERIKALI kupitia Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga kiasi cha Tsh.
Bilioni 5 katika mwaka 2016/17 zitazotumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
X-Ray katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
Hayo yalisemwa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya,
Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali
la Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua lini jengo la
Maabara ya Mionzi linalojengwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya litakamilika.
Ummy alisema katika
mwaka wa Fedha 2015/16 Tsh. Bilioni 8 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi huo,
ingawa ujenzi huo haukufanyika lakini nia ya Serikali ya kukamilisha ujenzi wa
jengo hilo uko pale pale.
Akiainisha matumizi
ya pesa zilizotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17, Ummy alisema Tsh. Bilioni 3
zitatumika kuendeleza ujenzi pamoja na kulipa deni lililobaki kwa mkandarasi
aliyekuwa anajenga na bilioni 2 zitatumika kununua vifaa tiba vikiwemo CT-
Scanner na MRI.
Akijibu swali la
nyongeza toka kwa Mhe. Catherine Magige (Viti Maalum CCM), Mkoa wa Arusha, Ummy
alisema bilioni 9 zimetengwa kwa ajili mya kununua vifaa tiba ikiwemo kuweka
CT-Scanner na MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Aidha Waziri Ummy
alisema kuwa Wizara imepata kibali cha kuajiri wafanyakazi 10,000 wa afya
nchini kati ya maombi ya kuajiri wafanyakazi 30,000.
Aliongeza kuwa
Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha
Hospitali za rufaa nchini ikiwemo ya Singida, Sekou Toure ya Mwanza, Mbeya na
Arusha.
Ummy alisisitiza kuwa
ni nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha sekta ya afya nchini na
kuwafanya wananchi kuwa na afya bora.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATENGA TSH. BILIONI 5 KUJENGA JENGO LA MIONZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.”
Post a Comment