Sunday, September 25, 2016

DAKTARI AUA MWANAFUNZI WAKATI AKIMTA MIMBA




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka minne jela, Daktari Nicholaus Matomola, baada ya kukiri kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Jubilate Shao, wakati akimtoa ujauzito.

Mahakama hiyo ilipewa kibali cha kusikiliza kesi ya mauaji ya bila kukusudia ili kupunguza mrundikano wa mahabusu, lengo likiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jitihada za kumaliza kesi zilizoko mahakamani kwa muda mrefu.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Msajili wa Mahakama Kuu, Mustapha Siyani, baada ya mshtakiwa kukiri kosa hilo.

0 Responses to “DAKTARI AUA MWANAFUNZI WAKATI AKIMTA MIMBA”

Post a Comment

More to Read