Saturday, October 29, 2016

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAIPIGA MWADUI FC 3-0







Simba imepata ushindi wake wa kwanza mbele ya Mwadui FC tangu timu hiyo inayomilikiwa na mgodi wa almasi ilivyopanda kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2015-2016. Simba imeifunga Mwadui magoli 3-0 kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kutoka na pointi tatu kwa mara ya kwanza dhidi ya Mwadui.

Kabla ya mchezo wa leo, Simba ilishindwa kupata ushindi katika mechi mbili za msimu uliopita huku ikichezea kichapo cha goli 1-0 kwenye uwanja wa taifa wakati wa mchezo wa marudiano. Mchezo wa kwanza uliozikutanisha klabu hizo ulipigwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga na Simba kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1.

0 Responses to “SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAIPIGA MWADUI FC 3-0”

Post a Comment

More to Read